Rais Ruto asema uchumi wa Kenya unakua vizuri
Rais William Ruto amesema kwamba serikali yake imedhibiti uchumi wa taifa na kwamba Wakenya wataanza kuvuna mazao ya mikakati iliyowekwa kuzuia gharama ya juu ya maisha mwezi ujao. Akiadhimisha mwaka moja tangu kuzinduliwa kwa hazina ya Hustler jijini Nairobi, rais alikosoa uamuzi wa kiuchumi wa serikali iliyopita akidai ulisababisha kuwepo kwa madeni mengi kupitia mikopo