Baadhi ya wabunge wa ODM kutoka Nyanza walalamikia Rais William Ruto kutowashirikisha kwenye ziara
Baashi ya Wabunge wa ODM kutoka eneo la Nyanza sasa wanalalamikia Rais William Ruto kutowashirikisha kwenye ziara yake inayokamilika leo katika eneo hilo. Wakiongozwa na mbunge wa kasipul Charles Were viongozi hao walilalamikia matamshi ya rais katika eneo la sindo kuhusu maandamano wakisema hayafai hawa wakati huu ambapo mazungumzo ya maridhiano yanaendelea.