1. Home
  2. William
  3. Ruto
  4. Rais William Ruto kuhutubia kongamano la Umoja wa Mataifa mjini New York

Rais William Ruto kuhutubia kongamano la Umoja wa Mataifa mjini New York

0
3

Rais William Ruto anatarajiwa kuhutubia mkutano wa baraza la usalama la umoja wa mataifa nchini Marekani mwendo wa saa tatu usiku wa leo.
Rais Ruto anatarajiwa kutumia fursa hiyo kuzungumzia sera za kigeni za Kenya zinazoangazia pia malengo ya maendeleo na usimamizi wa maswala ibuka ikiwemo mabadiliko ya tabianchi. Aidha, Rais atatumia fursa hiyo kuafiki uhusiano wa Kenya na Marekani. Rais aliondoka nchini Jumapili kuelekea Uingereza kwa mazishi ya Malkia Elizabeth wa Pili kabla ya kufululiza kwa mkutano huu maarufu wa UNGA jijini New York, Marekani .

Comment(3)

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *